Kocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson amefikia makubaliano na viongozi wa chama cha soka nchini humo juu ya kufutwa  kazi, endapo atashindwa kufikia malengo ya kufanya vizuri katika fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2016 ambazo zitaunguruma nchini Ufaransa.

Mtendaji mkuu wa chama cha soka nchini England FA, Martin Glenn amethibitisha makubaliano hayo yaliyofikiwa na pande zote mbili, kutokana na mikakati iliyowekwa ya kuhakikisha The Three Lion, hairejei makosa ya kufanya hovyo kama ilivyokua kwenye fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 kule nchini Brazil.

Glenn, amesema mazungumzo kati ya viongozo wa FA pamoja na Hodgson, yalianza tangu mwezi uliopita na kuna baadhi ya mambo yameafikiwa kutokana na maslahi ya soka la nchi hiyo, ambalo linahitaji kupiga hatua na kuondokana na kasumba ya kuwa wasindikizaji tangu mwaka 1966 ambapo walitwaa ubingwa wa dunia.

Amesema lengo kubwa lililopo kwa sasa ni kuiona timu ya taifa ya England inapiga hatua kubwa kwenye michuano ya barani Ulaya ya mwaka 2016, na ikiwezekana kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.

Katika mchakato wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Ulaya za mwaka 2016, timu ya taifa ya England ipo kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa kundi la tano ambalo lina timu za Uswiz, Slovenia, Lithuania pamoja na Sana Mrino.

Katika kundi hilo, England imesaliwa na michezo minne, ambapo Septemba 05 watapambana na San Marino Ugenini, Septemba 08 watacheza dhidi ya Uswiz nyumbani, Oktoba 09 watakwenda nchini Estonia kupambana na wenyeji kabla ya kumaliza mchakato wa kusaka tiketi ya nchini Ufaransa mwaka 2016 kwa kupapatuana na Lithuania Oktoba Oktoba 12.

Hisia Za Manyanyaso Ya kijinsia Zaibuka
Van Gaal Abadili Upepo Wa Usajili