Daktari wa klabu bingwa nchini England, Chelsea, Eva Carneiro ameamua kuondoka katika klabu hiyo wiki sita baada ya kukwaruzana na meneja wa timu, Jose Mourinho.

Carneiro aliingiliwa katika majukumu yake baada ya Mourinho kusema kuwa benchi lake la matibabu lilikuwa na watu wasiojua majukumu yao kwa kumtibu hovyo Eden Hazard wakati timu hiyo ilipotoa sare ya 2-2 na Swansea, Agosti 8.

Ingawa uongozi wa klabu ya Chelsea ulimuomba Carneiro mwenye umri wa miaka 42 kurejea kazini, daktari huyo mrembo alikataa na sasa analishughulikia suala hilo kisheria.

Chama cha Soka nchini humo FA, kinafuatilia malalamiko kwamba Mourinho alitumia lugha ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanadada huyo.

Hata hivyo, uongozi wa klabu ya Chelsea umesema kuwa hawana maoni juu ya masuala ya ndani ya watumishi.

Mwenyekiti wa ushirikishwaji wa bodi ya ushauri ya FA, Heather Rabbatts, ameelezea kusikitishwa kwake juu ya kuondoka kwa Carneiro.

CCM Yalalamikia Matokeo Ya Utafiti Wa Twaweza
Ni Mzunguuko Watatu Capital One Cup