Klabu ya Everton imeanza mazungumzo ya usajili wa kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa na Newcastle Utd Moussa Sissoko.

Taarifa kutoka jijini Paris nchini Ufaransa ambazo zimechapishwa katika gazeti la l’Equipe zinaeleza kuwa, The Toffees wameanza mazungumzo na wakala wa kiungo huyo ambaye ameonyesha nia ya kutaka kuondoka Saint James’ Park katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

Sissoko mwenye umri wa miaka 26, amekua akionyesha hisia za kutaka kuitumikia klabu ya Real Madrid kufuatia kila mara kuizungumzia klabu hiyo ambayo ilitwaa ubingwa wa barani Ulaya msimu wa 2015/16.

Hata hivyo Everton itawalazimu kujipanga kwa kutayarisha kiasi cha Pauni milioni 35 kama ada ya usajili ambayo tayari imeshatangazwa na uongozi wa Newcastkle Utd kama thamani sahihi ya Sissoko.

Hata hivyo Everton sio klabu pekee ambayo inatajwa katika harakati za usajili wa kiungo huyo ambaye alikua sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa wakati wa fainali za Euro 2016, pia ipo klabu ya Borussia Dortmund na Crystal Palace.

Klabu ya Borussia Dortmund inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Ujerumani, imejipanga kuingia katika dili la usajili wa Sissoko kwa lengo la kutanua kikosi chao kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Bundesliga mwishoni mwa juma lijalo.

Tayari wameshaanza kwa kumsajili kiungo kutoka nchini Ufaransa mwenye umri wa miaka 18 Ousmane Dembélé akitokea Rennes.

Mahrez Ategua Kitendawili, Ataja Klabu Anazozitamani
Yametimia - Jonathan Calleri Akabidhiwa Nyundo Za London