Klabu ya Everton itakosa huduma ya kiungo wake kutoka nchini Bosnia Muhamed Besic, kufuatia majeraha ya goti aliyoyapata wakati wa mchezo maalum wa kirafiki uliiochezwa usiku wa kuamkia jana dhidi ya Man Utd.

Taarifa zilizotolewa kwenye tovuti ya klabu ya Everton imeeleza kuwa, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 atakuwa nje ya uwanja hadi mwezi Februari mwaka 2017.

Besic, alidhaniwa huenda angekosa sehemu ya mwanzo ya msimu wa ligi ya nchini England ambayo itaanza mwishoni mwa juma lijalo, lakini baada ya kufanyiwa vipimo imebainika aliumia kwa kiasi kikubwa.

Muda mchache uliopita Besic, alithibitisha taarifa za jeraha linalomkabili kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter kwa kuandika (6 months out!) Nje kwa wa miezi sita!

Besic alibahatika kucheza michezo 12 ya ligi ya nchini England mwishoni mwa msimu uliopita, baada ya kujiuguza majereha misuli ya paja kwa muda mrefu.

Everton walicheza mchezo mchezo wa kirafiki dhidi ya Man Utd siku ya jumatano kwa ajili ya kumpa heshima mshambuliaji Wayne Rooney ambaye amebahatika kuchezea klabu hizo mbili.

Serengeti Yafungua Ukurasa Afrika Kusini, Wajue Nyota Wake
Hakuna Messi, Neymar Wala Suarez