Uongozi wa klabu ya Everton umekubali kumsajili beki kutoka nchini Argentina na klabu ya River Plate, Ramiro Funes Mori kwa ada ya paund million 5.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 24, anatarajia kuelekea nchini England kuimarisha soka lake la ushindani, huku akikatishiwa ndoto za kucheza nchini Hispania mbapo ilionekana dhahir huenda angesajiliwa na klabu ya Villarreal ambayo ilikua ya kwanza kuonyesha nia.

Sifa kubwa inayombeba Funes Mori hadi kufikia hatua ya kuwavutia viongozi wa klabu ya Everton, ni kuwa sehemu ya kikosi cha River Plate, kilichotwaa ubingwa wa Copa Libertadores mwaka huu.

Matarajio ya usajili wa Funes Mori, yanapewa kipaumbele zaidi huko Goodson Park kufuatia kuondoka kwa mabeki Sylvain Distin aliyejiunga na klabu ya Bournemouth pamoja na Antonio Alcaraz.

Wakati huo huo uongozi wa klabu ya Everton umeendelea kutilia mkazo wa kutokua tayari kumuuza mshambuliaji kinda John Stones ambaye anahitajika kwa hali na mali huko Stamford Bridge yalipo makao makuu ya klabu ya Chelsea.

The Blues wamekua wakijinasibu kuwa tayari kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21, kwa ada ya paund million 30 na wameshawasilisha ofa zaidi ya mara mbili lakini zote zimewekwa kapuni.

JK Anaamini Picha Za Mafuriko Ya Lowassa Zinatengenezwa
Soldado: Nilishindwa Kujiamini