Klabu ya Chelsea imeingia na uoga wa kukamilisha dili la beki kutoka nchini Senegal, na klabu ya Società Sportiva Calcio Napoli ya Italia Kalidou Koulibaly.

Taarifa zinaeleza kwamba, The Blues wameingai katika hali hiyo kufuatia uongozi wa klabu ya Everton kujitosa kwenye mipango ya kutaka ushindani wa kumuwania beki huyo mwenye umri wa miaka 25.

Klabu hiyo itakayoongozwa na Antonio Conte msimu ujao wa ligi kuu ya soka nchini England, tayari ilikua imeshawasilisha ofa ya Pauni milion 34 tangu juma lililopita, lakini walikutana na kizingiti cha ofa yao kuwekwa kapuni na viongozi wa SSC Napoli kwa kigezo cha kutokua na thamani dhidi ya Koulibalu.

Mmiliki mpya wa klabu ya Everton, Farhad Moshiri ameonyesha dalili za kuwa tayari kutoa kiasi cha Pauni milion 38, kama ada ya kumnasa beki huyo ambaye huenda akaweka rekodi ya kusajiliwa kwa gharama kubwa huko Goodson Park.

Everton wametangaza kuingia katika harakati za usajili wa Koulibaly, kufuatia uwezekano wa kuondoka kwa beki wao wa kati John Stones ambaye anawaniwa na matajiri wa mjini Manchester, Man City.

Borussia Dortmund Wapigana Kumrejesha Mario Gotze
Mama Ronaldo Ageuka Mbogo Kwa Payet