Klabu ya Everton inahusishwa na mpango wa kumrudisha aliyewahi kuwa meneja Roberto Martinez, baada ya kuachana na Meneja kutoka nchini Hispania Rafa Benitez.
Benitez alisitishiwa mkataba wake klabuni hapo mwanzoni mwa juma hili, kufuatia matokeo mabovu wa kikosi cha Everton katika michezo ya Ligi Kuu ya England.
Martinez anatajwa kwa asilimia kubwa kurejea klabuni hapo, licha ya majina ya mameneja wengine kuwa sehemu ya mchakato wa kumsaka Mkuu wa Benchi la Ufundi la the Toffees.
Wakati wa utawala wa Martinez, Everton iliwahi kumaliza katika nafasi ya tano ya katika msimamo wa Ligi Kuu ya England, ikiwa ni kubwa na ya mafanikio kwa klabu hiyo kuipata kwenye muongo mmoja uliopita.
Kwa mujibu wa BBC Sport, uongozi wa ‘ The Toffees’ umeanza hatua za awali za kumtoa Martinez kwenye kibarua chake cha kuiongoza timu ya Taifa ya Ubelgiji.
Wengine wanaotajwa kuwa sehemu ya kuwania kiti cha umeneja huko Everton ni Wayne Rooney, Frank Lampard na Duncan Ferguson.