Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji – EWURA, imevifungia kwa miezi sita Vituo vitatu vya uuzaji mafuta kwa muda wa miezi sita, baada ya kubainika kuficha mafuta kwa maslahi binafsi wakisubiri kupandishwa kwa bei kitu kilicholeta usumbufu kwa Wananchi na athari za shughuli za kiuchumi kwa jamii.

Mbele ya Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile  amesema hatua hiyo inatokana na changamoto ya uhaba wa mafuta iliyotokea Agosti na Septemba, 2023 ambapo baadhi ya wafanyabiashara walificha mafuta wakisubiria bei ipande, hivyo kuwapa Wananchi usumbufu na kuathiri zmshughuli zao.

Kwa mujibu wa Sheria ya Petrol sura Na 392 Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA ), imepewa jukumu la kudhibiti masuala ya mafuta pamoja na mambo mengine kuhakikisha kuna upatikanaji wa mafuta wakati wote na imepewa mamlaka ya kuwajibisha Vituo vinavyokiuka taratibu za leseni zao.”

Vituo hivyo vilivyofungiwa ni Camel Oil- Gairo Petrol Station chenye leseni namba PRL 2019-164, PETCOM-Mbalizi Petrol Station chenye Lessen namba PRL 2023-025 na  Rashal Petroleum Ltd – Mkalama chenye Leseni namba PRL 2019-034, huku vitatu vikiendelea kuchunguzwa.

Amesema, EWURA imevichukulia hatua vituo vinane ambavyo vilihodhi mafuta ambapo Septemba 4, 2023 pia ilivifungia vituo viwili vya CAMEL Oil cha Msamvu Morogoro  na kile cha Matemba  kilichopo Turiani na kwamba vingine vitatu vipo katika uchunguzi.

Lamine Yamal awekewa ulinzi mkali
Daktari Mtibwa Sugar afunguka hali ya Makaka