Chama cha soka nchini England FA, kimesema kitachunguza kwa kina tukio lililojitokeza katika uwanja wa klabu ya Tottenham Hotspurs, wakati wa mchezo wa mzunguuko wa tatu wa kombe la ligi nchini humo *Capital One Cup* uliochezwa usiku wa kuakia jana baina ya wenyeji dhidi ya Arsenal.

Mashabiki wanaodhaniwa kuwa ni wa klabu ya Arsenal wanadaiwa kufanya uharibifu kwenye sehemu ya uwanja wa White Hart Lane, kutokana na furaha ya ushindi wa mabao mawili kwa moja waliokua wameuvuna ugenini.

Mashabiki hao walidaiwa kuchana mabango yaliyokua yamebandikwa sehemu ya majukwaa ambayo yalibeba ujumbe wa kauli mbinu ya Spurs isemayo To Dare Is To Do.

Tayari jeshi la polisi jijini London limethibitisha kuwashikilia mashabiki 10 wanaituhumiwa kufanya tukio hilo, ambalo lilionekana kuwakera viongozi pamoja na mashabiki wa Spurs.

Katika mitandao mbali mbali ya kijamii na ile ya habari, picha za tukio hilo zimeanikwa hadharani kuthibitisha namna uharibifu huo ulivyofanywa kwa makusudi.

Ngebe, Majivuno, Tambo Kumalizwa Kesho Taifa Stadium
Malinzi Awalilia Mahujaj Waliopoteza Maisha Saudia Arabia