Baadhi ya klabu za ligi kuu ya soka nchini England, zimefahamu wapinzani wao katika mzunguuko wa pili wa michuano ya kombe la ligi EFL Cup (English Football League).
Klabu za Liverpool, Chelsea pamoja na Everton ni sehemu ya klabu shiriki za ligi kuu ya soka nchini England ambazo zitaanza kuonekana katika mzunguuko wa pili wa michuano hiyo.
Liverpool watapambana na Burton Albion ugenini, Chelsea watakuwa nyumbani wakimsubiri mshindi wa mchezo kati ya Bristol Rovers na Bristol City huku Everton watapapatuana na Yeovil katika uwanja wa Goodison Park.
Liverpool walifahamu mapema kama wangecheza mchezo huo ugenini kutokana na ombi lao kupokelea vyema na chama cha soka nchini England FA, kufuatia matengenezo ya jukwaa kuu ambayo yatakuwa yakifanyika mwishoni mwa mwezi huu katika uwanja wa Anfield.
Kikosi cha Jurgen Klopp kitalazimika kucheza kwa malengo makubwa ili kurekebisha makosa yao ya msimu uliopita, baada ya kushindwa kumaliza vyema kwenye mchezo wa hatua ya fainali dhidi ya Manchester City, ambao walichomoza na ushindi wa mikwaju ya penati.
Michezo ya mzunguuko wa pili wa michuano ya kombe la ligi EFL Cup (English Football League), imepangwa kuchezwa Agosti 23 na 24, na ratiba kamili inayonyesha kuwa:
QPR v Rochdale
Scunthorpe v Cardiff/Bristol City
Watford v Gillingham
Peterborough v Swansea
Everton v Yeovil
Millwall v Nottingham Forest
Sunderland v Shrewsbury
Luton v Leeds
Chelsea v Bristol Rovers/Bristol City
Burton v Liverpool
Blackburn v Crewe
Accrington v Burnley
Crystal Palace v Blackpool
Morecambe v AFC Bournemouth
Preston v Oldham
Oxford v Brighton
Reading v MK Dons
Fulham v Middlesbrough
Newcastle v Cheltenham
Exeter v Hull City
Derby v Carlisle
Northampton v West Brom
Wolves v Cambridge
Stevenage v Stoke
Norwich v Coventry