Chama cha Soka nchini Uingereza FA kimesema kuwa kitatunga sheria kali za kuwashughulikia wachezaji wenye tabia za kujirusha hovyo wawapo uwanjani kwa lengo la kupoteza muda ama kudanganya ameumia.
Aidha. FA imesema sheria hiyo itaanza kutumika mara moja mara baada ya kukamilika katika msimu ujao ili kuweza kukabiliana na wachezaji ambao wamekuwa wakifanya hivyo kwaajili ya kupoteza muda na kudanganya kuwa wameumia.
FA imesema mara baada ya kukamilika kwa sheria hiyo na kuanza kutumika, kabla ya adhabu kutolewa kutakuwa na jopo la maamuzi ambalo litaongozwa na mwamuzi, meneja wa timu na mchezaji husika aliyetenda kosa hilo.
Hata hivyo, FA imesema kama mchezaji atabainika kuwa amedanganya katika tukio husika basi adhabu yake itakuwa ni kufungiwa michezo miwili.