Beki wa pembeni kutoka nchini Ureno, Fabio Coentrao atajiunga kwa mkopo na klabu ya AS Monaco ya nchini Ufaransa, baada ya viongozi wa klabu ya Real Madrid kukubali kufanyika kwa dili hilo.

Coentrao, mwenye umri wa miaka 27, ataelekea nchini Ufaransa kwa mkataba wa mkopo wa muda mrefu hivyo anatarajiwa kucheza ligi ya nchini humo katika kipindi chote cha msimu wa 2015-16.

Maamzi ya kumtoa kwa mkopo beki huyo, yamefikiwa kufuatia ruhusa iliyotolewa na meneja wa Real Madrid, Rafael Benitez ambaye amesisitiza kutokua na mpango na Coentrao.

AS Monaco wanaamini Coentrao, matawasaidia katika kipindi chote cha msimu huu, ambapo wamedhamiria kurejesha ushindani wa kuwani ubingwa wa nchini Ufaransa ambao unashikiliwa na PSG.

Tayari klabu ya AS Monaco imeshapoteza nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu, baada ya kukubalia kichapo cha jumla ya mabao 4-3 dhidi ya Valencia, licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa mkondo wa pili.

U-15 Yajifua Morogoro
Stars Kupambana Na Libya Kesho