Mtandao wa Facebook umeondoa video ya aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump kwenye ukurasa wa mkwe wake Lara Trump.

Facebook ilimpiga marufuku Trump kutumia mtandao wake mnamo mwezi Januari, kufuatia ghasia zilizosababishwa na wafuasi wake katika jengo la Capitol mjini Washington.

Lara Trump, mchambuzi mpya wa shirika la habari la Fox News, aliweka video ya yeye mwenyewe akimhoji Trump kuhusiana na masuala mbalimbali.

Kufuatia marufuku aliyowekewa Donald Trump katika mtandao wa Facebook na Instagram, ujumbe wowote utakaowekwa wenye sauti ya Donald Trump utafutwa na matokeo yake itakuwa kuendelea kuongezwa kwa masharti.

UEFA wafanya mabadiliko EURO 2020
Mjumbe Simba SC amkingia kifua 'Mo'