Bingwa wa WBC Afrika nchini na Bondia namba moja Tanzania, Fadhili Majiha ‘Kiepe Nyani’ ameweka rekodi ya kuwa bondia wa kwanza kupata hadhi ya nyota nne na nusu tangu nchi ipate uhuru huku akivunja rekodi ya Hassan Mwanyiko na Tony Rashid katika mtandao wa boxrec.

Majiha ameweka rekodi baada ya juma moja tangu ashinde mkanda wa ubingwa wa Afrika kwa kumchapa kwa pointi Bongani Mahlangu wa Afrika Kusini katika pambano la raundi kumi ambalo lilipigwa kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar.

Majiha au Kiepe Nyani ambaye asili yake ni mkoa wa Lindi katika Wilaya ya Ruangwa, mbali ya kufikisha nyota hizo nne na nusu lakini ameingia katika orodha ya mabondia kumi bora duniani akiwa kwenye nafasi ya saba katika mabondia 1056 wa uzani wa Bantam.

Ikumbwe kuwa bondia Hassan Mwakinyo ndiye bondia wa kwanza nchini kufikia hadhi ya nyota nne pamoja na kuingia kwenye kumi bora ya dunia uzani wa Super Walter kwa kukaa katika nafasi ya tisa kabla ya Tony Rashid kufutia kwa kufikisha nyota tatu na nusu na kuingia kwenye 20 bora ya dunia ya uzani wake wa Super Bantam yenye mabondia 1248.

Mafanikio ya Majiha yamekuja baada ya kuchukuliwa na Kampuni ya HB Sadc Boxing Promotion ambayo ndiyo waliohusika kumuandalia pambano lake la kuwania mkanda wa ubingwa wa WBC Afrika dhidi Bongani licha ya mtandao wa boxrec kuonekana kwa majina ya Mghana, Azumah Cofie ambaye jina lilikuwepo baada ya Majiha kumtwanga Harvey Uingereza, Novemba 25 mwaka jana.

Majiha ambaye ameomba kupata nafasi ya kupeleka mkanda wake wa ubingwa wa WBC Afrika kwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan kama zawadi yake kutokana na kuwa bondia wa kwanza nchini na Afrika kushinda mkanda wa ubingwa huo.

Parimatch, Tigo Pesa wazindua promosheni Vibunda Spesho
Ahmed Ally: Tumebaki na maumivu ya kudumu