Katika biashara ni kawaida kukutana na wateja wa aina tofauti tofauti na hutakiwi kumpa mteja wako huduma vibaya hadi ajisikie kwamba hataweza tena kuja kwenye biashara yako.

Mteja anatakiwa kujaliwa na kupewa huduma ambayo itamfanya ajione kwamba yeye ni mfalme kwa mazingira yoyote yale uliyo.

Fahamu aina hii ya wateja

1. Wateja wanaolalamika sana.
Wapo wateja ambao kazi yao ni kulalamika sana. Wateja hawa wanalalamikia kitu hiki au kile kwenye biashara na kushindwa kuongea ukweli na kutatua changamoto za pamoja. Wateja hawa ni hatari sana kwenye biashara yako.

2.Wateja wanaotaka kupatanisha kila kitu
Sina shaka unawajua wateja ambao ukiwatajia bei ya kitu, wao ni kutaka kupatanisha na kuomba punguzo kila wakati. Unapokuwa na wateja wa namna hii wengi basi biashara yako itakuwa na usumbufu sana.

Hawa ndio wateja ambao unatakuiwa kuwaepuka au kuwa nao makini sana kwenye biashara yako. Sijasema wateja hawa uwafukuze au uwajibu vibaya, ila unatakiwa kuwa nao makini ili wasije wakakuvurugia wateja wengine ambao ulitakiwa kuwa nao kwenye biashara.

3.Wateja wanaojiona wao ni maalumu sana                                               
Kuna wateja ambao wanapenda kujiona wao ni muhimu sana kuliko wateja wengine. Wateja hao ni rahisi tu kudai namba ya meneja wako au bosi wako ili wamweleze kile wanachokitaka wao wenyewe.

Unachotakiwa kuwa makini nacho hapa ni kuwa makini na wateja wa namna hii unapokutana nao ana kwa ana na hata wale unaokutana nao kwenye mitandao. Fanya hivi bila wao kujua kwamba unawaepuka.

Adam Mchomvu amuomba radhi Rais Magufuli
Kenya: Mawaziri, makatibu kuchukua likizo ya lazima