Bamia ni mboga maarufu hapa Tanzania mbali na kuwa na ladha nzuri, lakini pia bamia ina faida mbalimbali za kiafya kwa mwili wa mwanadamu.

Watu wengi hutumia bamia mara chache sana licha kutokana na kiungo hicho kutokupendwa licha ya bei yake kuwa rahisi.

Wtaalamu wa afya na lishe wanasema kuwa walaji wa bamia wananufaika kwa kupata maelfu ya viini lishe vinavyopatikana kwenye zao hilo kiwemo kuongeza utimamu wa mapigo ya moyo.

Zifuatazo ni faida za kula bamia

Ulaji wa bamia husaidi wanawake kuepukana na changamoto za kiafya hasa wanawake wanaopata shidaya hedhi mara kwa mara bila kufikisha hata angalau siku 24 nadani ya mwenzi mmea huu unauwezo wa kufiisha tatizo hilo.

Virutubisho vinayopatikana katika bamia vinauwezo wa kupambana na magonjwa ya kujamiiana, zao hili linasaidia katika kutibu magonjwa mbalimbali ya zinaa kama vile kaswende, kisonono.

Bamia husaidia kutibu vidonda vya tumbo kwa kusawazisha kemikali inayotemwa tumboni, lakini pia husaidia kushusha sukari hadi kiwango cha chini, Angalizo kwa wagonjwa wa kisukari, msiache dawa zenu na kuanza kutumia bamia kama dawa.

Vitamini C inayopatikana katika bamia husaidia watoto wanaougua ugonjwa wa pumu kupumua vizuri wanapotumia zao hili.

Faida nyingine ya ulaji wa bamia ni kuusaidia mwili kusafisha damu, ulaji wa bamia husaidia kutibu tatizo la upungufu wa damu lakini pia ulaji wa bamia pia huondoa sumu mwilini.

Watu wenye matatizo ya vidonda vya tumbo, bamia huwasaidia kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya tumbo na huongeza kiwango cha damu mwilini.

Hii ndiyo faida ya kunywa maziwa
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 22, 2020