Dengue ni ugonjwa unaosababishwa na virusi viitwavyo Dengue vinavyosambazwa na mbu aina ya Aedes.
Mbu huyu hupendelea kuishi karibu na makazi ya watu na huweza kuuma binadamu mchana na usiku.
Mtu anaweza kutambua kuwa anamaambukizi ya homa hii kwa kuwa na dalili hizi; Homa kali ya ghafla, Maumivu makali ya kichwa, Macho kuuma, Maumivu ya viungo, Kichefuchefu, Kutapika, Vipele ambavyo hutokea siku nne baada ya homa kuanza, Kutoka damu puani, kwenye fizi na kuchubuka kirahisi
Mara nyingi dalili huwa sio kali na wengi hudhania ni homa ya mafua au maambikizi mengine ya virusi.
Dalili hizi huanza kutokea baada ya wiki mbili, lakini kwa wengi huchukua wiki moja ya kwanza na tayari utaanza kuona dalili za dengue.
Matatizo yanayoweza kutokea baada ya maambukizi ya homa ya Dengue ni pamoja na Homa kali zaidi, Kuharibiwa kwa tezi na mishipa ya damu, Kutokwa na damu zaidi puani na kwenye fizi, Ini kuwa kubwa na huweza kupelekea kifo.
Kutokana na gharama kubwa ya kufanya vipimo vya ugonjwa huo sasa Serikali imeagiza baadhi ya hospitali za umma kufanya kipimo hiko bure, Mganga Mkuu aetaja baadhi ya hospitali itayofanya vipimo hivyo bure ni pamoja na Amana, Mwananyamala, Mnazi Mmoja, Bombo na hospitali ya mkoa wa Singida.