Ugonjwa wa Kaswende ni moja ya magonjwa ya zinaa yanayosababishwa na bakteria aina ya spirochetes wasioweza kuishi muda mrefu wakiwa nje ya mwili wa binadamu wanaoitwa Trepenema pallidum.

Mwaka 1943 iligunduliwa dawa aina ya Penicillin ambapo kwa kiasi kikubwa ilisaidia kupungua kwa kwa maambukizi ya ugonjwa huo duniani japokuwa maeneo ya Kusini mwa Jangwa la Sahara, China, Marekani ya Kusini mashariki mwa bara la Asia bado ugonjwa huo ni tishio kubwa.

Utafiti uliofanya unaonyesha kwamba asilimia 2 mpaka 20 ya  wamama wanaoenda kupimwa kipindi cha ujauzito hukutwa na kaswende lakini pia ugonjwa huu umetapakaa sana maeneo ya mijini ukilinganisha na vijijini.

Kaswende inaweza kusambaa kwa njia kadhaa kama ifuatavyo; ngono, mama mjamzito kwenda kwa mtoto kupitia kondo la uzazi, kubadilishana damu, kubusiana kwa mdomo, kubadilishana mate.

Unaweza kufahamu kuwa unamaambukizi ya ugonjwa huu kwa kuwa na dalili zifuatazo.

Vipele mwilini ambavyo hutokea baada ya miezi sita na kusambaa sehemu za uke, puru, mikononi, miguuni, kifuani, mgongoni na hata usoni, upele huu hauwashi na kipindi hiki mgonjwa anakua hatari sana kwani huweza kuambukiza mtu kwa kumkumbatia au kumshika tu.

kidonda kisichokua na maumivu hutokea baada ya siku 10 mpaka 90 baada ya kupata maambukizi, kidonda hicho hakina maumivu na hukaa siku chache na kupotea bila matibabu, kidonda hiki hutokea pale wadudu walipoingilia huweza kuwa kwenye uume, uke, mdomoni, kwenye maziwa na kadhalika

Lakini pia dalili nyingine ni, kuvimba kwa sehemu za siri pamoja na mdomo, maumivu ya kichwa pamoja na viungo, homa, kupungua kwa uwezo wa kusikia, kuona na uwiano wa mwili.

Baada ya mwaka mpaka miaka kumi ugonjwa huu usipotibiwa huingia ndani ya mwili na kushambulia mishipa ya fahamu na ubongo mgonjwa huanza kuonyesha dalili za ugonjwa wa akili na wakati mwingine mtu huwa kichaa kabisa.

Na endapo usipofanya matibabu ya ugonjwa huu unaweza kusambaa hadi kwenye moyo, na viungo vingine vya mwili na hata kusababisha kifo.

Wanawake wajawazito wanaweza kujifungua watoto wenye kasoro za viungo na pia mimba zinaweza kutoka

Watoto wachanga wanaozaliwa na kaswende wanaweza kufa ama kupatwa na ulemavu wa kudumu kama vile wa kutoona.

Kw mujibu wa utafiti uliofanywa na madaktari wa magonjwa ya zinaa Australia.

 

CWT yaiunga mkono Serikali kuboresha Miundombinu ya Elimu
Video: JPM abariki bakora za RC, Jinsi msajili anavyoweza kumchomoa Mbowe