Baada ya kusubiri kwa muda mrefu, hatimaye klabu ya Liverpool imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL), msimu huu 2019/20.

Ndoto ya miaka 5 ambayo walikuwa wameiota kwa kumchukua meneja kutoka Ujerumani Jurgen Klopp akitokea Borrusia Dortmund imefanikiwa kujibu bila shaka, baada ya msimu uliopita kuachwa kwa alama chache na waliokua mabingwa Manchester City.

Majogoo wa Jiji la Merseyside walifanikiwa kutwaa taji la EPL bila kukanyaga uwanja, kwani baada ya mchezo wao dhidi ya Crystal Palace walioshinda mabao manne kwa sifuri Jumatano iliyopita, walihitaji alama mbili pekee kuwa mabingwa, lakini balaa lililomkuta aliyekua bingwa mtetezi Manchester City mbele ya Chelsea likawa faraja kwao.

Dar 24 kwa kushirikiana na Meridianbet tumeandaa kipindi (meridianbet SPORTS) maalum cha kuizungumzia Liverpool FC sambamba na kuwapongeza mabingwa hao wapya wa EPL, ambao walisiburi kwa takriban miaka 30, kutwaa taji la ufalme wa soka England. Kwa kuangalia kipindi cha meridianbet SPORTS bofya video hapo chini.

Mingange: Simba SC walistahili ubingwa
Atakayeamua Simba SC Vs Azam FC huyu hapa

Comments

comments