Kumiliki gari ni kitu ambacho vijana wengi wanatamani kutokana na adha ya usafiri hasa jijini Dar es salamm ambako kuna usafiri mgumu wa kutumia daladala hivyo vijana wengi wakipata kazi inayowalipa mshahara mnono cha kwanza hufikiria kununua gari.
Hivyo wakati unafikiria kununua gari fikiria pia ipo siku utahitaji kubadilisha gari hiyo, kuna mambo ya msingi ambayo watu wengi wamekuwa wakiyapuuza na athari zake huonekana baadae pale ambapo wanataka kuchukua hatua fulani dhidi ya gari hilo.
Mambo haya apa muhimu ya kuzingatia wakati wa kununua gari ambapo watu wengi huyapuuzia na kufanya makosa.
- Fikiria kuhusu mauzo ya gari lako pindi utapotaka kuliuza ili ubadilishe gari jingine, hapa kikubwa kinachoangaliwa ni jina la gari, kuna magari magumu sana kuingia sokoni na kununulika hii ni kutokana na upatiakanaji wa vifaa vya ziada pindi gari hilo linapokuwa limeharibika, pia inashauriwa zingatia rangi ya gari yako ambapo watu wengi hupendelea gari rangi nyeusi, silva na nyeupe.
- Gharama za matengenezo ya gari unalotaka kununua ikiwa pamoja na gharama za mafuta ya gari. Gharama za matengenezo ya gari hupanda mwaka kwa mwaka kutokana na huduma mbalimbali zinahitajika kufanyika kwenye gari hilo kwani kadri siku zinavyoenda ndivyo matengenezo ya gari yanakuwa makubwa. Ni vizuri kufikiria ni kiasi gani cha fedha kinaweza kutumika kwa matengenezo na huduma nyingine muhimu za gari ili lisikushinde na uweze kusogeza mambo mengine katika familia.
- Kununua toleo jipya la gari, haishauriwi sana mtu kununua toleo jipya la gari, kwani watengeneza magari hutengeneza magari na kuayapa muda wa majaribio ili kufanya maboresho zaidi katika toleo lijalo, hivyo inashauriwa kununua magari yaliyotoka kuanzia miaka mitatu iliyopita.
- Sio kila mwezi ni mwezi wa kununua magari inashauriwa miezi mizuri ya kununua gari ni kuanzi mwezi wa 12 mpaka mwezi wa 3 ili kuokoa kiasi fulani cha pesa kwani miezi hii kampuni mbalimbali zinazofanya mauzo ya magari kwa kutoa ofa ya kushusha bei ili kuuza bidhaa zao.
- Cha mwisho, Usiwe na haraka ya kununua gari fanya tafiti sehemu mbalimbali, watumie watu wanaojua juu ya magari wakushauri juu ya gari unalotaka kununua kusanya taarifa mbalimbali sehemu tofauti tofauti kisha fanya maauzi sahihi, usikurupuke.