Tazama mambo 5 yenye mvuto juu ya urembo wa mwanamke uliokuwa unatumika miaka ya zamani kabla ya vita vya dunia, kuna baadhi ya vitu vya urembo kama rangi ya mdomo ‘Lipstick’ wanja wa machoni ‘mascara’, manukato, rangi za kucha vilianza kutumika tangu miaka ya zamani ambapo kila urembo uliokuwa unatumika ulikuwa na maana fulani sio kama hivi sasa.
1. Lipstiki ndio urembo pekee uliokuwa ukitumika wakati wa vita vya dunia hasa na wauguzi ili kuwa na mvuto na kuwatibu wanajeshi waliokuwa wakipata majereha wakati wa vita vya pili vya dunia na wanajeshi hao waliamini kuwa kutibiwa na mwanamke mwenye rangi ya mdomoni hupata nafuu mapema na kurudi vitani.
2. Upande wa kushoto wa uso wako unasemekana kuwa ndio upande wenye uzuri kuliko upande wa kulia wa uso wako.
3. Egypt miaka ya nyuma walikuwa wakitumia manukato kama dawa ya kutibu magonjwa ya mapafu, utumbo pamoja na ini.
4. Kwa mara ya kwanza rangi ya kucha iligundulika nchini China mwaka 300 BC ambapo walitengeneza kwa kutumia n’ta ya nyuki, gundi, yai na unga wenye rangi.
5. Revlon ndio ”brand” ya kwanza kutengeneza na kupeleka sokoni rangi nyekundu ya kucha duniani.