Nanasi lina vitamin A, B, C lakini pia lina madini ya chuma, calcium, phosphorus na copper. Pindi mtu atumiapo tunda hili  lina uwezo mkubwa wa kuimarisha  mifupa, meno. Misuli na neva za mwili.

Ingawa wapo baadhi ya watu huwa hawapendi kutumia tunda hili kwa madai kuwa linawasha kwenye ngozi maeneo ya mdomo mara baada ya kulitumia, inawezekana watu hao wakawa sawa ila ukweli ni kwamba achana na kuwasha kwa mdomo bali wewe angalia faida zitakonazo na tunda hilo.

Zifahamu faida za kula tunda la nanasi mwilini.

1. Husaidia kwa kiwango kikubwa kwa wale wenye matatizo ya choo, lakini pia inashauriwa ya kwamba kwa wakina mama wajawazito na wale wanyonyeshao walitumie nanasi kwa wingi kwa sababu  lina faidakwa mtoto.

2. Kwa wale wenye matitizo ya athma pia wanashauriwa walitumie tunda hili kwani lina uwezo wa kutibu ugonjwa huo.

3. Nanasi ni miongoni mwa matunda ambayo yana uwezo wa kurudisha kumbukumbu, hivyo basi kwa wale ambao wana matatizo haya  ya kupoteza kumbukumbu wanashauriwa kutumia tunda hili.

4. Wale wenye matatizo ya utumbo mwembamba na magonjwa ya koo wanashauriwa watumie tunda hili kwani husaidia sana kutibu magonjwa hayo.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 26, 2020
Rais wa Uturuki atilia shaka afya ya akili ya Macron

Comments

comments