Kimsingi ndoto ni hadithi na picha ambazo hutengenezwa na akili zetu wakati tukiwa usingizini, ndoto zinaweza kukufurahisha, kukuhuzunisha au kukuogopesha.
Wataalamu wanadai tunapata ndoto nne hadi sita ndani ya usiku mmoja.
Faida za ndoto kiafya ni kama kuamsha ubunifu, unapoota ndoto taarifa ulizojifunza hivi karibuni na zile ulizojifunza zamani hugongana na kuunda taarifa mpya bora zaidi hivyo kukufanya uamke na masuluhisho bora zaidi ya changamoto mbalimbali.
Pia ndoto hutibu hisia na akili, kupitia ndoto tunaweza kutoa hisia zote mbaya kama hasira tulizopata siku nzima.
Ukiwa ndotoni unaweza kupata ahueni ya kihisia hivyo kukufanya uamke ukijihisi vizuri baada ya mahangaiko ya kihisia kama mahusiano kuvunjika.