Homa ya Ini ni ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya virusi ambavyo vikiingia mwilini hushambulia ini na virusi hivyo huitwa HBV (Hepatitis B Virus), ni moja ya ugonjwa hatari zaidi na unaopoteza maisha ya watu wengi kwa kasi kubwa zaidi.
Tafiti zinaonyesha kasi ya ugonjwa huu ni ya hatari zaidi kuliko hata ya Ukimwi kwa sababu virusi vya Hepatitis B vinaweza kuishi nje ya mwili wa binadamu (yaani nje ya mfumo wa damu) kwa siku saba ambapo Virusi vya Ukimwi (VVU) havina uwezo wa kuishi nje ya mfumo wa damu hata kwa dakika moja.
Watu takriban 1,000,000 wanapoteza maisha duniani kote kutokana na ugonjwa wa Homa ya Ini (Hepatitis B) na mara nyingi endapo ugonjwa huu haujatibiwa hutengeneza uvimbe katika ini na kusababisha kansa ya ini na baadae kifo.
-
Fahamu dalili, matatizo yatokanayo na dengue
-
‘Dkt. Mwaka’ aeleza alivyofanya mazingaombwe hadi kuwa Tabibu
Kama ilivyo kwa Ukimwi, Virusi vya Homa ya Ini pia huambukizwa kwa njia ya kujamiiana, mate, jasho na mwingiliano wowote ule wa damu, Mama mwenye ugonjwa kumwambukiza mtoto wakati wa kujifungua, Kuchangia damu isiyo salama, Kuchangia vitu vya ncha kali kama sindano, wembe, Kuchangia miswaki, kuchangia taulo na mwenye ugonjwa huo, kubadilishana nguo au kukumbatiana wakati mkiwa mnavuja jasho.
Kwa wastani kirusi cha HBV kikishaingia mwilini, hupevuka ndani ya siku 75, hata hivyo upo uwezekano wa kupevuka kati ya siku 30 hadi 180. Ndani ya siku 30 mpaka 60, mtu mwenye HBV anaweza kugundulika ikiwa atapimwa.
Mtu mwenye Homa ya Ini ana wastani mdogo wa kuishi kuliko mwenye Ukimwi. Kwa maana hiyo, mwenye maambukizi ya Virusi vya Homa ya Ini hufariki dunia haraka kuliko mwenye VVU.
Watu wengi hawaonyeshi dalili yoyote. Kwa maana hiyo mtu anaweza kuishi na HBV na kusababisha maambukizi kwa wengine bila kugundulika.
Japokuwa watu wengine husumbuliwa na homa kali na dalili ambazo hudumu kwa wiki kadhaa dalili hizo ni Uchovu
Kichefuchefu, Mwili kuwa dhaifu, Homa kali, Kupoteza hamu ya kula, Kupungua uzito, Maumivu makali ya tumbo, upande wa ini, Macho na ngozi kuwa vya njano, Mkojo mweusi.
Kwa wagonjwa wengine, Virusi vya Hepatitis B hukua hadi kusababisha ini kuharibika kabisa (cirrhosis of the liver) au saratani ya ini (liver cancer).
Mpaka sasa Homa ya Ini haina tiba, vilevile hakuna dawa maalum za kurefusha maisha. Ugonjwa huo ukishafikia kiwango cha ini kuharibika au kupata saratani ya ini, maana yake kinachofuata ni kifo.
Namna ya kujikinga na ugonjwa huu ni pamoja na Chanjo, Kutumia kinga wakati wa kujamiana, Kuacha kuchangia, vitu vya ncha kali kama sindano, wembe, Kutochangia miswaki, Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu, Kutochangia damu isiyo salama.
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), Kusini ya Jangwa la Sahara ndiyo eneo hatari zaidi.
Tanzania ni moja ya nchi zilizopo katika eneo hilo, Kiwango cha hatari Kusini mwa Jangwa la Sahara kinalingana na kile cha Mashariki ya Bara la Asia.
Ripoti hiyo inaonesha kuwa watu wengi walipata maambukizi nyakati za utotoni na kwamba kati ya asilimia tano mpaka 10 ni waathirika sugu.