Tafiti zinaonesha omba omba tajiri duniani wanapatikana katika jimbo la Oregon nchini Marekani, katika hali ya kawaida omba omba jimboni humo hujipatia takribani dola 300 za kimarekani kwa siku ambayo ni sawa na shillingi laki 6 na 70 elfu za kitanzania.
Uhalisia ambao ni tofauti na tamaduni za Kitanzania, gharama hiyo kitanzania ni sawa na mshahara wa mtu mwenye elimu ya chuo kikuu.
Hii inadhihirisha Tanzania ni nchi maskini, ambapo omba omba wengi wa kitanzania huambulia sarafu kadhaa ambazo haziwezi kukishi mahitaji yao kama binadamu.
Matokeo yake, Tanzania inaweza kuwa ni nchi inayoongoza kwa uhalifu mdogomdogo, umaskini kutokana na kukosa kazi za kufanya kujipatia kipato.
Serikali na jamii kwa ujumla wanajukumu la kuhakikisha mtanzania mmoja kwa siku anajipatia kiasi cha fedha kujikimu na maisha ili kuepusha vijana kujiingiza katika utafutaji riziki usio wa uhalali.