Juni 19 ni siku ya siko seli duniani, ugonjwa ambao mtu hupata kwa kurithi ambapo mwathirika huwa na himoglobini ‘’S’’ ambayo hupeleka chembe hai nyekundu za damu zisizo za kawaida kushindwa kupita kwenye mishipa ya damu kirahisi na kupelekea kuwa na upungufu wa damu kwenye baadhi ya sehemu mwilini.

Kwa kawaida seli nyekundu za damu huwa na umbo la duara\mviringo lakini mtu aliyeathirika na ugonjwa wa siko seli au selimundu seli zake nyekundu za damu huwa na umbo la mwezi mchanga au mundu.

Katika andiko hili ni vyema kufahamu kuwa kuna aina tatu za seli mundu kitaalamu ipo seli mundu ya sickle cell anemia (ss), sickle beta plus na sickle hemoglobin (sc) na magonjwa yote hayo hugundulika kwa kufanyiwa kipimo kiitwacho hemoglobin eloctrophonesis.

Kubwa la kufahamu kuhusu ugonjwa huu ni kwamba ni ugonjwa unaorithiwa na si ugonjwa wa kuambukizwa.

Siko seli au seli mundu ni miongoni mwa magonjwa yanayoendelea kutikisa nchi mbali mbali duniani ambapo kila mwaka watoto Laki tatu huzaliwa na ugonjwa huo wa kurithi, ambapo Kati ya hao, asilimia 80 wanatoka barani Afrika.

Tanzania ni nchi inayoshika nafasi ya nne kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa. Nigeria ikiwa kinara inashikilia nafasi ya kwanza, ikifuatiwa na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na ya tatu ni Angola.

Kwa mtu mzima utamgundua kuwa na dalili za siko siko seli kwa kuona mabadiliko haya ambayo si ya kawaida kwa mwili wa mgonjwa, Upungufu wa damu, Maumivu ya tumbo, Maumivu ya mifupa (viungo), Kupooza, Maumivu ya kifua yafananayo na nimonia (acute chest syndrome), Kubana kwa kifua, Kukojoa damu, Vidonda sugu miguuni, Kusimama kwa uume kuambatanako na maumivu makali (priapism), Kuvimba kwa paji la uso au fuvu.

Hakuna tiba ya moja kwa moja ya kuponya ugonjwa siko seli au selimundu mgonjwa hutakiwa kupata matibabu kwa kipindi chache chote cha maisha yake na hutakiwa kutumia dawa kila siku hata wakati wanapokuwa na afya nzuri ambapo matibabu yanaweza kuwa ni chanjo ya kuzuia magonjwa fulani, dawa za kuzuia sumu ya maambukizo, chanjo ya kuboresha utengenrzaji wa seli nyekundu za damu.

Aidha mgonjwa wa siko seli anatakiwa kuepuka kukaa maeneo yenye joto sana au baridi kali, anatakiwa kunywa maji mengi angalau glasi 8 kwa siku, kutumia chakula chenye lishe bora, kupumzika vizuri na kupata usingizi mwingi, kuonana na daktari mara kwa mara.

 

Misri yaunyoshea kidole Umoja wa Mataifa kuhusu kifo cha Morsi
Merkel aikomalia Iran kuhusu mashambulizi ya meli