Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru ametangaza rasmi kuwa waombaji mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2018/2019 dirisha la uombaji mikopo kwa njia ya mtandao kwa mwaka wa masomo 2018/2019 litafunguliwa kuanzia Alhamisi, Mei 10, 2018 hadi Jumapili, Julai 15, 2018.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilianzishwa chini ya kifungu cha sheria namba 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi Julai, 2005. Bodi ya Mikopo pamoja na majukumu mengine ina jukumu la kutoa mikopo au ruzuku kwa wanafunzi wenye sifa na wahitaji.

Wanafunzi watakaopatiwa ruzuku kwa mwaka wa masomo 2018/2019, waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu, lazima watimize vigezo vilivyowekwa, Bonyeza linki hapo chini kufahamu vigezo muhimu vinavyohitajika kwa muhitaji wa mkopo wa masomo ya Elimu ya juu.

HESLB

 

Watu 3 wafariki dunia kwa ajali, 11 wajeruhiwa vibaya Dar
FC Barcelona waanza mikakati ya kumsajili Griezmann