Hakuna kitu kinachomnyima mtu raha akiwa mbali na maeneo yake aliyoyazoea kama simu kutokuwa na chaji, na mbaya zaidi mtu huyo awe ametembea bila chaji ya simu yake.
Siku hizi tumeona muda mwingi watu wengi hupoteza wakiwa na simu zao wakifanya vitu mbalimbali, wengine simu ndio ofisi yao yaani kwa kutumia simu zao wanaweza kufanya na kukamilisha majukumu mbalimbali ya kiofisi.
Hivyo basi wengi wanaomiliki simu hawawezi kukaa zaidi ya dakika 10 bila kushika simu zao, hivyo suala la chaji linanyima raha watu wengi na hivyo hulazimika kutembea na chaji ili wanapopata nafasi ya kuchaji waweze kuchaji simu zao.
Watengenezaji wa simu wengi hasa hizi simu janja za kuteleza maarufu kama ”Smart phone” wemeshindwa kwa kiasi kikubwa kutengeneza simu zenye uwezo mkubwa wa kukaa na chaji.
Japo kampuni kama Tecno, Infinix wamejaribu kutengeneza betri imara ambazo kwa kiasi fulani zinajitahidi kukaa muda mrefu bila kuzima.
Hivyo basi kwa wale watumiaji wa simu zenye majina makubwa kama vile Samsung, na Apple nimewaletea mambo makubwa matano yatakayosaidia simu yako isiishiwe chaji kwa uharaka zaidi ambayo watu wengi wamekuwa wakiyapuuzia lakini kwa kiasi kikubwa humaliza chaji za simu.
1. Uwashaji wa bluetooth, wengi wanapowasha bluetooth za simu zao husahau kuzizima mara baada ya kumaliza kutumia mfumo unaosaidia kubadilishana vitu kutoka simu moja kwenda simu nyingine.
2. WI-FI, hii ni maalumu kwa ajili ya kutumia interneti ya mtu mwingine endapo atakuwa amewasha kitu kinachoitwa Hot spot.
3. Mwanga wa simu- blightnes.
4. Vibration- mngurumo.
5. Wallpaper zinazobadilika.
Hivyo ili kuepuka kumaliza chaji katika simu yako, yaepuke mambo ambayo nimeyaainisha hapo juu.