Kipimo cha IQ ni njia pekee inayoaminiwa kupima uwezo wa akili za mtu ambapo kwa kawaida binadamu wengi wana IQ ya kuanzia 90 mpaka 110 lakini watu wachache sana wana IQ level ya kuanzia 140 na kuendelea.

Wapo wanyama pia ambao wametambulika kuwa miongoni mwa wanyama wenye akili zaidi duniani kutokana na mienendo yao.

Utafiti uliyofanywa na Chuo Kikuu cha New York Marekani umegundua wanyama wenye akili karibiana na binadamu ambapo utafiti huo ulionesha jinsi gani mazingira wanayoishi yanavyowafanya kuwa wenye akili.

Hawa hapa ndiyo wanyama 10 wenye akili zaidi duniani.

  1. Tembo wana akili kubwa kuliko mnyama yeyote wa ardhi kavu, tembo ana uwezo wa kutafuna majani ya dawa kuanzisha uchungu wa kuzaa, kutambua vitu kwenye kioo, kuigiza sauti mbalimbali na kutumia vitu mbalimbali kwa matumizi sahihi pasipo kufundishwa, pia ndiyo wanyama pekee wanaoweka msiba pale mwenzao anapokufa.

2. Pweza

Ana uwezo wa kutoroka akikamatwa na kufungiwa kwenye mzingile (maze) ana ubongo mkubwa kuliko wanyama wote wasio na uti wa mgongo lakini pia wana uwezo mkubwa wa kujua maadui, ndio mnyama pekee wa kundi hilo kutumia zana, hujibadili kukwepa maadui, mfano mzuri ni Pweza Paulo aliyetabiri Hispania kuchukua kombe la dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini.

3. Njiwa

Ana uwezo wa kutambua herufi zote 26, ana uwezo wa kurudi nyumbani hata akiwa kilomita mia kutoka nyumbani na ndiyo sababu walikuwa wanatumika kutuma ujumbe kwa wauza madawa ya kulevya pia wanatumika kuuza madawa hasa magerezani.

4. Mbwa

Ni marafiki wakubwa wa binadamu, ambapo mbwa wa kawaida ana akili sawa na mtoto wa binadamu mwenye umri wa miaka miwili, wana uwezo mkubwa wa kunusa harufu, kujilinda, na kujifunza kutoka kwa binadamu.

5. Panya

Ana uwezo wa kuhesabu, kutambua muda, kuwasiliana na wenzake na kuwa na uhusiano mzuri na binadamu kama anafugwa.

6. Sokwe

Ana uwezo wa kujifunza kutamka baadhi ya maneno kuwasiliana na wenzake kutumia vitu kwa matumizi yake sahihi na huwa anaumia pale mwenzake anakufa.

7. Nguruwe

Wanatunza kumbukumbu kwa muda mrefu, wana uwezo wa kuwasiliana na wenzake na ndiyo mnyama msafi zaidi katika wanyama wanaofugwa.

8. Nyangumi

Ndiyo mnyama mwenye ubongo mkubwa zaidi kama ilivyo Pombo, nyangumi anaweza kuwasiliana na wenzake na kwa sauti mbalimbali na kujifunza pia.

9. Kasuku

Anaweza kujifunza maneno, herufi na namba uwezo wake kiakili unafanana na binadamu wa miaka minne.

10. Pombo

Hawa kwa lugha ya kingereza hufahamika kama Dolphins ni wanyama ambao binadamu huwatumia kutatua matatizo mengi hususan ya baharini. Akili ya pomboo ni kubwa kama miili yao, huonyesha hisia mbalimbali, hujifunza vyema mazingira yao, nusu tu ya akili yake hulala, nusu nyingine ikiwa macho kukabiliana na tishio lolote.

Spurs yapigwa 3-0, Connolly atakata
Video: Tazama hapa wimbo mpya wa Rayvanny 'Chuchumaa'