Leo tutaangazia ulaji wa tende, na kuzingatia kuwa huu ni mwezi Mtukufu wa Ramadhani ndiyo tunda ambalo huliwa kwa wingi, pengine kuliko tunda lingine.
kisayansi, tunda hilo limethibitika kusheheni madini na vitamini nyingi kiasi cha kulifanya liwe na faida nyingi kiafya, fahamu faida hizi 7 mwilini.
- Husaidia kuongeza sukari kwa mtu aliyefunga
Mtaalamu wa Lishe, Juliana Majaliwa anasema mtu aliye kwenye mfungo, mara zote huwa kiwango chake cha sukari mwilini hupungua na hutakiwa airejeshe tena kwa kula vyakula mara tu anapotakiwa kufuturu.
Hivyo, ulaji wa tende mtu anapo futuru, humfanya asijihisi kuchoka sana na huwa na nuru zaidi ya macho. Pia tende husaidia kuimarisha na kuboresha mfumo wa usagaji wa chakula tumboni, hivyo ni rahisi kuondokana na matatizo ya ukosefu wa choo au matatizo ya kupata choo kigumu kinachosababisha maumivu wakati wa kujisaidia.
Pia tende husaidia kupata virutubisho vya ‘amino acids’ ambavyo ni muhimu mwilini, pia mwili kutapata aina mbalimbali za madini na vitamin za kutosha, ambazo zinapatikana kwenye tunda hili maarufu ambalo lina kiasi kidogo cha mafuta yasiyo na lehemu.
-
Zijue faida za parachichi katika kulinda afya yako
-
Je unafahamu faida za pilipili hoho mwilini, hizi hapa 7
Ingawaje tende mara nyingi si chakula kinachopendelewa sana na watu wenye njaa, lakini ndicho chakula kisicho na mafuta na ni chanzo madhubuti cha sukari.
Wataalamu wa lishe wanasema mfungaji akila tende, atajipatia kiasi cha kutosha cha protini na vitamin B1, B2, B3, B5, A1, na C, virutubisho ambavyo ni muhimu kwa ustawi wa afya ya mwili kwa ujumla.
2. Tende husaidia kuimarisha moyo.
Inashauriwa kuiloweka tende kwenye maji kwa usiku mmoja na asubuhi kunywa maji hayo pamoja na tende zilizolewekwa baada ya kuondoa mbegu, ukifanya hivyo mara mbili kwa wiki, moyo wako utakuwa imara.
3. Wenye matatizo ya kukauka damu
Wataalamu wanasema kwa mfungaji mwenye tatizo la kukauka damu mwilini (anemia), anaweza kupata ahueni kwa kula tende kwa wingi ambayo ina kiwango cha kutosha cha madini ya chuma ambayo huhitajika katika utengenezaji wa damu mwilini. Wakati vitu vingine vitamu vinadaiwa kuwa huozesha meno, lakini wataalamu wa tiba lishe wanasema utamu wa tende huzuia uozaji wa meno.
4. Huondoa tatizo la nguvu za kiume
Kwa matatizo ya ukosefu wa nguvu za kiume, mchanganyiko maalum wa tende, maziwa, asali na unga wa hiriki vinaweza kuondoa tatizo hilo. Chukua kiasi cha kiganja kimoja cha tende, loweka kwenye maziwa ya mbuzi kiasi cha lita moja, ziache zilowane kisha zisage kwenye maziwa hadi zichangayike, weka vijiko vitatu au vinne vikubwavya asali pamoja na nusu kijiko cha chai cha hiriki, kisha kunywa mchangayiko huo kila siku hadi utakapoona mabadiliko ya kuridhisha.
5. Tende ni dawa
Tunaelezwa kuwa tende ni dawa ya unene na kwa wale wenye matatizo ya wembamba wa kupindukia na wanataka kuongeza uzito, ulaji wa tende kila siku unaweza kuwasaidia. Lakini hii ina maana wale wanaohitaji kupunguza uzito, ulaji wa tende kwa wingi hauwezi kuwafaa, Mtaalamu wa tiba ya mimea, Japhet Lyatuu, anasema tende hutibu pia saratani ya tumbo na
6. Husaidia pia kuondoa hali ya ulevi
kwa wale wanaokunywa pombe, matumizi ya tende mara kwa mara husaidia kukata hamu ya kutumia kilevi cha aina yeyote.
7. Tende husaidia kuchelewesha dalili za uzee
Kwani husaidia kurekebisha ngozi na kuondoa mabaka ya kuungua na jua.