Wengi tumekuwa tukitumia kama mboga au kiungo kimoja wapo katika kunogesha mboga lakini wachache mno wanaojua faida za nyanya chungu kiafya.
Nyanya chungu ipo kwenye kundi la mbogamboga zenye virutubisho vingi ikiwemo vitamin A, B, na C ambazo zote kwa pamoja hufanya kazi ya kuobresha afya ya mwili kwa ujumla.
Zifahamu faida mbili za matumizi ya nyanya chungu.
Ngogwe au nyanya chungu husaidia sana katika kuongeza nguvu za uzazi kwa wanaume na inatibu pia wale wenye ugonjwa wa ngiri.
Hizi pia ni kinga inayoweza kumwepusha mlaji kupata maradhi ya moyo. Kwa wagonjwa wa kisukari nyanya chungu pia ni dawa inayoweza kusaidia katika kupunguza kiwango cha sukari ndani ya mwili.
Mbali na sifa hiyo ya ngogwe / nyanya chungu pia husaidia kuongeza stamina na uwezo wa kuvumilia na kudumu kwenye tendo la ndoa kwa muda mrefu kati ya mume na mke wote endapo watakuwa wanatumia nyanya chungu katika utaratibu unaotakiwa kitaalam (mchemsho) .
Mbali na hayo, ngogwe ni dawa inayofanana na antibiotic, hivyo ni tunda zuri endapo likitumiwa mara kwa mara husaidia kuua vijidudu vya aina mbalimbali mwilini.
Vitamin K inayopatikana ndani ya nyanya chungu inasaidia kuipa nguvu mishipa ya damu hivyo kusaidia zoezi zima la mzunguko wa damu katika mwili wa binadamu.
Licha ya kuwa karibu asilimia 90 ya nyanya chugu ni maji mboga hii pia inajumuisha madini ya chuma na potassium.