Kutoka nchini Marekani bado headlines zinayashikilia maendeleo ya sakata la muigizaji Will Smith kumcharaza kofi mchekeshaji Chris Rock wakati wa utolewaji wa tuzo za Oscar usiku wa kuamkia Machi 28, 2022 katika ukumbi wa Dolby huko Los Angeles.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka kwa vyanzo vya kuaminika inaelezwa kuwa baada ya tukio hilo mchekeshaji Chris Rock amepata mafanikio kwa kiasi kikubwa kutokana na umaarufu wake kuongezeka maradufu baada ya kupigwa kofi na Will Smith.

Miongoni mwa matunda yanayotajwa kuyapata mchekeshaji huyo ni pamoja na kuuza tiketi zote za onyesho lake la vichekesho alilopanga kulifanya katika maeneo mbali mbali kwa kuanza na Aprili 2, 2022 huko New Jersey nchini Marekani.

Ripoti zinasema kuwa onyesho hilo alilolibatiza jina la ‘Ego Death Comedy Tour’ limefanikiwa kupata muitikio mkubwa na kwamba viti vyote tayari vimelipiwa kutokana na shauku ya watu kutaka kumuona nyota huyo aliyekuwa sehemu ya mjadala mkubwa kote duniani.

Kabla ya ziara hiyo kuanza Chris Rock amepanga kufanya onyesho la ufunguzi katika ukumbi wa Wilbur huko Boston na tiketi za onyesho hilo licha ya kuongezwa bei lakini zimeuzwa kwa wingi na kuisha mapema tangu kuanza kuuzwa kwake.

Kwa mujibu wa kampuni ya Tick PickĀ  inayojihusisha na uuzaji wa tiketi za maonyesho mbali mbali imechapisha taarifa yake kwenye mtandao wa twitter ikieleza kwamba wamefanikiwa kuuza tiketi nyingi zaidi kwa watu waliodhihirisha wazi kuwa wenye shauku ya kutaka kumuona Chris Rock akichekesha.

Kinu cha nyuklia Ukraine chaachiwa huru na Wanajeshi wa Urusi
Habari Picha:Rais Samia akiongoza kikao ca kamati kuu pamoja na halmashauri kuu ya CCM taifa