Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa damu kwenye viungo vya uzazi, kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi.

Sifa kuu za kitunguu saumu zinazokifanya kuwa na uwezo na faida nyingi mwilini ni kuwa na viasili kadhaa ambavyo vina uwezo tofauti tofauti.

Baadhi ya viasili hivi husaidia kutanuka kwa mishipa ya damu ( vasodilation kwa lugha ya kiingereza) kwa kubadilisha polysulphides zilizo ndani yake kuwa hydrogen sulphides kwenye seli nyekundu za damu.

Pia, kitunguu saumu husaidia kuthibiti kiwango cha kemikali iitwayo homocystine mwilini na hivyo kupunguza madhara ya kisukari.

Kuwa na damu ya kutosha katika uume husababisha hiki kiungo kusimama na hivyo kustaimili tendo la ndoa kwa muda mrefu.

Namna ya kutumia kitunguu swaumu:

Unashauriwa kuchukua vipande vya kitunguu saumu kisaha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10, meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala.

Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.

Wataalamu wanashauri kufanya hivi kila baada ya siku 1 unapoenda kulala kwa wiki 3 mpaka 4.

 Ukiona kichwa kizito au kinauma pumzika kutumia kitunguu swaumu kwa siku 3 hivi kisha endelea tena, muhimu usitumie kila siku bali ni kila baada ya siku 1.

Rais Samia awasili Uganda
Serikali yaahidi kukamilisha mradi wa JNHPP