Hatimaye Shindano la Bongo Star Search (BSS) msimu wa nane, jana (Oktoba 9) limempata mshidi wa msimu wa nane aliyeondoka na shilingi milioni 50, Kayuma Juma.

Kayumba ambaye ni mkazi wa Temeke, Dar es Salaam mwenye umri wa miaka 19 alifanikiwa kuwashawishi watanzania wengi pamoja na Majaji wa shindano hilo hivyo ushindi wake ulipokelewa kwa mikono miwili na watu wengi zaidi.

Nassib Fonabo alishika nafasi ya pili kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuimba na kupiga gitaa. Machaguo ya nyimbo zake kubwa zilipelekea kusifiwa sana lakini nyimbo hizo huenda zilikuwa hazieleweki kwa baadhi ya wapiga kura.

Nafasi ya tatu ilienda kwa mshiriki kutoka Arusha, Frida Amani ambaye mtindo wake wa kurap ulikuwa kivutio kwa wengi tangu alipoanza mashindano hayo. Frida alitolewa wakati wa mchujo wa Top 5, lakini kwa maombi maalum ililazimika kuingiza watu sita badala ya watano kama ilivyokuwa imepangwa awali.

 

Msemo wa ‘Hapa Kazi Tu’ Wamgharimu MC wa Bongo Star Search
Angalia Orodha Ya Wachezaji Walevi Duniani