Kulikuwa na uvumi mkubwa juma lililopita kwamba uamuzi FIFA wa kukabidhi haki za kuandaa Fainali za Kombe la Dunia la 2030 kwa mataifa sita katika mabara matatu inamaanisha kuwa michuano ya mwaka 2034 itakuwa ya kuvutia endapo Saudi Arabia itapewa uenyeji.
vyanzo vilivyo karibu na Saudi Arabia vimeliambia gazeti la MailSport kwamba FIFA inapanga kulipa uenyeji taifa hilo lenye nguvu kifedha mwaka 2034 huku ikidaiwa mchakato na makubaliano yanaenda vizuri.
Katika hali ya kushangaza Jumatano ya juma lililopita, FIFA ilitangaza kwamba Uruguay, Argentina na Paraguay kila moja itakuwa mwenyeji wa moja ya mechi tatu za ufunguzi katika Kombe la Dunia la 2030.
Miaka 100 iliyopita baada ya Uruguay kuandaa Kombe la Dunia la kwanza. Sasa mataifa hayo matano yamepewa nafasi ya kuwa wenyeji wa michuano hiyo mikubwa duniani.
Naye Sheik Salman kutoka Bahrain, mtu mwenye nguvu zaidi katika soka la bara la Asia, alitangaza: “Familia nzima ya soka ya Asia itasimama kwa pamoja kuunga mkono mpango muhimu katika Ufalme wa Saudi Arabia, na tumejitolea kufanya kazi kwa karibu na familia ya soka duniani kuhakikisha mafanikio yanapatikana.”
Hatua hiyo imewakera Australia kwani wana mapango wa kuwania uenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2034 baada ya kuandaa fainali za Kombe la Dunia la Wanawake mwaka huu.
Lakini Saudi Arabia itapata kura nyingi ndani ya bara la Asia na nyingine kutoka bara la Afrika hivyo Australia inaamini haitapata nafasi. Rais wa FIFA, Gianni Infantino pia yuko karibu na mfalme mteule ‘Mohammed bin Salman.