Faiza  Ally, amefunguka Kuhusu kulizwa na harusi ya Sugu huku akidai kuwa yalikuwa ni machozi ya furaha baada ya kuona baba mtoto wake anafunga ndoa.

” Siku ile nililia kwa sasababu nilihisi mzigo niliokuwa nimeubebeba miaka mingi nimeuvua” amesema Faiza

Ameongeza kwa Mara nyingi akiwa kwenye furaha au kwenye huzuni huwa anachanganya kucheka na kulia, “sikuwa nimelia kwa uchungu nimeendelea na maisha yangu”.

Faiza amesema kuwa yeye huwa yupo huru kwenye maisha yake kwasababu anauwezo wa kutafuta pesa na ana uwezo wa kufanya chochote ambapo amesema alikuwa anaenzi penzi lake la zamani kwa njia ya huzuni.

Pia faiza amesema licha ya mwanae Sasha kuwa na mawasiliano na baba yake kupitia simu aliyomnunulia yeye hana mawasiliano kabisa na mzazi mwenzie Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu.

lakini hajaishia hapo ameikosoa hadhi Hoteli ya mzazi mwenzie huyo kwa kulinganisha na hoteli nyingine alizo wahi kutembelea.

”Hoteli ya Sugu ni ya kawaida sana kwa nchi za watu ile sio hoteli” amesema mrembo huyo na kuongeza kuwa ameanza kutembea  akiwa chini ya umri wa  miaka 20 kwenye nchi za watu.

Mavunde ajipanga kuboresha sekta ya Elimu Dodoma
Mambo 7 kujikinga na ugonjwa wa kichaa cha mbwa