Mwili wa Rosemary Nyerere ambaye ni mtoto wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, utazikwa Jumatano ya Januari 6, 2021, katika makaburi ya Kituo cha Hija, Pugu jijini Dares Salaam.

Rosemary alifikwa na mauti Ijumaa Januari Mosi 2021 katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa muda mrefu akipatiwa matibabu.

Rosemary ambaye alizaliwa mwaka 1961 aliwahi kuwa mbunge wa Bunge la Muungano katika Bunge la 9 na enzi za uhai wake alisema akifariki azikwe makburi hayo ya Pugu.

Kwa sasa msiba uko Msasani jijini Dar es Salaam, nyumbani kwa Mwalimu Nyerere, ambako watu mbalimbali wakiwemo viongozi wanakwenda kutoa salamu za pole kwa wafiwa.

Majaliwa aagiza kukamatwa madiwani watatu
Zidane akataa kumpumzisha Benzema