Msanii mkongwe wa muziki wa dansi nchini Mzee King Kiki ambaye pia ni msemaji wa familia ya Nguza Viking maarufu kama Babu Seya, amesema kuwa familia hiyo inataka kukutana na Rais John Pombe Magufuli kwa lengo la kumshukuru.

Ni kufuatiwa na uamuzi alioutoa Rais Magufuli mnamo Disemba 9, 2017 kuwaachia uhuru baadhi ya wafungwa wakiwemo Nguza Viking na mwanaye Johnson Nguza baada ya kutumikia kifungo cha jela kwa zaidi ya miaka 10.

“Saizi Nguza na Papii wapo kwenye mapumziko lakini wanapaswa kurudi nyumbani Congo kwenda kutekeleza mambo ya kimila, hivyo hawapaswi kufanya jambo lolote lile kwa sasa mpaka wakamilishe hilo suala la kimila, ila kabla ya wao kuondoka tumekuwa tukiomba kama tunaweza kupewa nafasi ya kuonana na Mhe. Rais kumshukuru na kumpa ahsante itakuwa ni vizuri sana kabla ya wao kwenda nyumbani” alisema Mzee King Kikii

Nguza na wanawe watatu walikamatwa Oktoba 12, mwaka 2003 na kufikishwa Kituo cha Polisi Magomeni, Dar, walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Oktoba 16, mwaka 2003 wakituhumiwa kubaka na kunajisi watoto 10.

Baada ya kusikilizwa kesi hiyo Juni 25, 2004, Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar, Addy Lyamuya aliwatia hatiani Babu Seya na wanaye kifungo cha maisha kwenye Gereza la Ukonga, Dar es Salaam.

 

 

 

Aliyeongoza Jeshi kumng’oa Mugabe apewa ‘Tonge Nono’
George Weah atangazwa mshindi wa Urais Liberia