Wakati ikiwa katika majonzi mazito kuelekea siku rasmi ya kumpumzisha mpendwa wao, familia ya marehemu ‘AKA’ imeridhia na kuthibisha ujio wa Album mpya ya nyota huyo iitwayo ‘Mass Country’.

Hii ni kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na familia hiyo kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za marehemu AKA, huku ikibainishwa wazi kuwa sababu za kuachiwa kwa album hiyo ni kuheshimisha jitihada za marehemu katika kila alichowahi kuthubutu kukifanya kwenye muziki na mchango wake kwa ujumla.

Kwa mujibu wa familia, album hiyo ni miongoni mwa album ambazo AKA aliwekeza akili na nguvu kubwa katika maandalizi yake muda mfupi kabla ya kukutwa na umauti.

Familia ya AKA katika maombolezo

“Alijitahidi kufanya kazi kubwa kwenye mradi huu, alihakikisha anawekeza moyo na akili yake katika hii album na kizuri ni kwamba alipata nafasi ya kuikamilisha yote na kuikagua katika kila kipengele, hivyo kitakachotoka kitakuwa kwa mujibu wa muongozo na mtazamo wake yeye mwenyewe.” imesema familia ya AKA.

Familia ya kijana aliyeuawa pamoja na AKA yatoa tamko

Pamoja na taarifa hiyo ya ujio waa a album ya nyota huyo ambaye uhai wake ulikatishwa kwa kushambuliwa kwa Risasi mwishoni mwa juma lililopita huko Darbun nchini Afrika kusini, familia pia imethibitisha ujio wa wimbo mmoja utakaotangulia kuachiwa uitwao ‘Company’ aliomshirikisha mwimbaji Kiddominat.
Wakati ikiwa katika majonzi mazito kuelekea siku rasmi ya kumpumzisha mpendwa wao, familia ya marehemu ‘AKA’ imeridhia na kuthibisha ujio wa Album mpya ya nyota huyo iitwayo ‘Mass Country’.

Hii ni kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na familia hiyo kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za marehemu AKA, huku ikibainishwa wazi kuwa sababu za kuachiwa kwa album hiyo ni kuheshimisha jitihada za marehemu katika kila alichowahi kuthubutu kukifanya kwenye muziki na mchango wake kwa ujumla.

Kwa mujibu wa familia, album hiyo ni miongoni mwa album ambazo AKA aliwekeza akili na nguvu kubwa katika maandalizi yake muda mfupi kabla ya kukutwa na umauti.

Rapa AKA enzi za uhai wake

“Alijitahidi kufanya kazi kubwa kwenye mradi huu, alihakikisha anawekeza moyo na akili yake katika hii album na kizuri ni kwamba alipata nafasi ya kuikamilisha yote na kuikagua katika kila kipengele, hivyo kitakachotoka kitakuwa kwa mujibu wa muongozo na mtazamo wake yeye mwenyewe.” imesema familia ya AKA.

Pamoja na taarifa hiyo ya ujio waa a album ya nyota huyo ambaye uhai wake ulikatishwa kwa kushambuliwa kwa Risasi mwishoni mwa juma lililopita huko Darbun nchini Afrika kusini, familia pia imethibitisha ujio wa wimbo mmoja utakaotangulia kuachiwa uitwao ‘Company’ aliomshirikisha mwimbaji Kiddominat.

Mkutano AU: Rais Samia awasili nchini Ethiopia
Serikali yataka kasi ujenzi uwanja wa Ndege Msalato