Familia ya Babu Seya imeeleza kuwa tukio la kuachiwa huru kwa mzee Nguza Viking (Babu Seya) na mwanaye Johson Nguza lilitabiriwa na Nabii.

Akizunguza jana katika ibada ya Kanisa la Life In Christ Ministry Zoe lililopo Tabata jijini Dar es Salaam, mtoto wa Babu Seya, Michael Nguza (Nabii Nguza) alisema kuwa Mchungaji wa Kanisa hilo, Nabii Joseph alitabiri mara tatu kuwa wanamuziki hao wataachiwa huru.

“Utabiri wa kwanza ulikuwa mwaka 2012, wa pili mwaka 2014 na wa tatu ni Mei 21 mwaka huu. Alisema watu wawili ambao ni baba na mwanaye wataachiwa huru, mmoja ni kijana na mwingine ni mzee,” alisema Nabii Nguza.

Alisema kuwa kila aliposikia utabiri huo alikuwa anapeleka ujumbe huo kwa ndugu zake hao gerezani.

Babu Seya na wanaye walifungwa jela maisha baada ya kukutwa na hatia ya kuwabaka na kuwalawiti watoto 10 wa kike, waliokuwa wanafunzi wa shule ya msingi Mashujaa, Sinza jijini Dar es Salaam.

Baada ya kukaa gerezani kwa miaka 13, Disemba 9 mwaka huu, Rais John Magufuli aliwataja kuwa miongoni mwa wafungwa waliopata msamaha wa Rais.

Babu Seya na mwanaye walifika katika kanisa hilo na kuombewa na Nabii Joseph muda mfupi baada ya kutoka katika gereza la Ukonga.

Dkt. Shein awatahadharisha wanaodhani ni mpole
Magazeti ya Tanzania leo Desemba 25, 2017