Familia za waandishi wa habari watatu waliofariki kwenye ajali iliyotokea Januari 2022, wamelipwa kiasi cha Tshs. Milioni tano kila moja ikiwa ni malipo baada ya kujiunga na mfuko huo yanayotolewa na benki ya Tanzania Commercial Bank (TCB) kwa kushirikiana na Kampuni ya Bima ya Alliance Insurance.

Akiongoza zoezi hilo Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi, ambaye amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel, amewahamasisha waandishi wa habari kujiunga na mfuko huo kwani una faida mbalimbali ambazo zinamfariji mwanachama akipata madhila na majanga

Katika kuainisha majanga hayo yanayoshughulikiwa na bima ni kama vile ulemavu na kifo na mwandishi au familia atalipwa mkono wa pole.

Bima hiyo inalipa endapo akifariki mwanachama, familia yake italipwa Tshs. Milioni 5, akifiwa mke au mume, atalipwa Tshs. Milioni 4, akifiwa watoto, atalipwa Tshs. Milioni 2 na akifiwa baba, mama na wakwe, atalipwa Tshs. Milioni 1.

Tukio hilo lilihudhuriwa na familia za wafiwa, waandishi wa habari wa Mwanza, Viongozi wa dini, wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan.

Familia za wafaidika wa bima hiyo ya ‘Nishike mkono’ ni kutoka kwa waliokuwa Wanachama Marehemu Johari Shani, Anthony Chuwa na Husna Mlanzi, kati ya Wanachama 31 wa “Wanahabari Bima Group”.

Simba SC kuweka kambi Morocco
Mtibwa Sugar yamjibu Haji Manara