Kila mtu amekuwa na dhana yake tofauti katika kutasfiri dhana ya urembo kuna wanaojua kuwa ili kuwa mrembo basi ni alazima uwe na ngozi nyeupe au nywele ndefu au umbo lako liwe la kuvutia, lakini sio kweli, urembo ni vile wewe unajiweka ili kuwa nadhifu na kuwa na muonekano wa kuvutia hata kama uwe mwembamba kiasi gani au mweusi kiasi gani.
Kwanza jiaminishe kuwa wewe ni mrembo kuliko watu wanavyokuchukulia fanya yafuatayo:
1:Safisha ngozi yako kila siku.
katika kusafisha ngozi kuna mambo mengi, jitahidi kuifanya ngozi yako kuonekana nyororo na safi muda wote, hii itakusaidia kuonekana mrembo kwa asilimia zote. Ondoa ngozi iliyokufa , sugua ngozi ili kuondoa mafuta na uchafu unakuwa umeganda katika ngozi yako, hii unaweza kuifanyika kwa masaage au kufanya scrub mwili.
jaribu kuchangua bidhaa bora za kutumia katika kusafisha ngozi yako usizisahau nywele zako kila wakati, zitunze na uzipende hata kama ni fupi kwani urembo sio sura tu bali kila sehemu ya mwili wako inapokuwa safi inarekebisha muonekano wako.
2.Fanya mazoezi
Mazoezi yanakufanya uwe mkakamavu siku zote , lakini pia mazoezi yanasawazisha mwili na kufanya uwe na umbo la wastani lenye muonekano wa kuvutia katika vitu vinavyochangia afya ya ngozi na urembo ni mazoezi.
3.Epuka vipodozi vya mara kwa mara.
Kuna watu wamezoea kupaka vipodozi kila muda, wanafanya ngozi muda wote kuwa imefungana na kukosa hewa ya kutosha sio kila kipodozi ni urembo vingine uharibu ngozi yako onana na wataalamu wakupe ushauri juu ya kipodozi gani sahihi cha kutumia.
Mara nyingi vipodozi vyenye kemikali viansababisha kulegea kwa ngozi, lakini pia vile vinavyochubua ufanya wanawake wengi kushindwa kushonwa wakati wa kujifungua hasa kwa wale wanaohitajika kufanyiwa operation, ngozi kuungua na kushindwa kukaa juani.
4.Jitahidi kupata usingizi wa kutosha
Sio kwa afya ya mwili na akili tu , bali usingizi wa kutosha usababisha mtu kuonekana mrembo, kulala kwa muda unaofaa kuna kufanya usionekane mchovu na macho yako yanakuwa angavu siku zote.