Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amewataka Wakuu wapya wa Wilaya kuacha kufanyakazi kwa ‘kiki’ za ajabu za kuwakamata watu na kuwaweka ndani masaa 48 bila sababu kunaweza kupelekea watu kuichukia Serikali yao.
Amesema kuwa sheria zinaruhusu lakini ni pale ambapo jinai inatakiwa itendeke machoni pa Mkuu wa Wilaya, kwa kuzuia hilo jambo lisitendeke ndio Mkuu wa Wilaya anatakiwa atumie Sheria hiyo.
Aidha, ameongeza kuwa Mkuu wa Wilaya anasikia jambo limetokea mahali tofauti na alipo anatoa maagizo kuwa huyo weka ndani, hiyo inasababisha chuki zisizo na maana kwa kutumia huko sheria vibaya.
“Unakuta leo hii Mkuu wa Wilaya anamuweka ndani mtu au mtumishi wake kwa sababu ambazo hata hazina tija, eti tu kwa sababu walishagombana huko nyuma na yeye anatumia mamlaka yake kulipa kisasi.”amesema Jafo
-
Mwakyembe ataka watanzania wanaolipishwa na StarTimes kupeleka ushahidi
-
Video: Waziri Mkuu awataka viongozi wabadilike kimtazamo, kihoja, kiushauri na utoaji maamuzi
-
Video: kazi niliyotumwa ni hii, hayo ndiyo mambo natakiwa nifanye – Jerry Muro
Hata hivyo, amewaasa Wakuu hao wa Wilaya kutumia sheria ipasavyo ili kuzuia athari kubwa ambayo inaweza kutokea