Beki wa kimataifa wa Algeria anayekipiga na klabu ya SSC Napoli, Faouzi Ghoulam ameongeza mkataba na klabu yake utakaomuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2022.

Mkataba wa sasa wa mlinzi huyo unamalizika tarehe 30 ya mwezi june mwaka 2018, hivyo mkataba mpya umeongeza miaka minne ya wa kukipiga na vinara wa Seria A.

Ghoulam kwa sasa anauguza jeraha la goti alilofanyiwa upasuaji baada ya kuumia katika mchezo wa ligi ya mabingwa wa ulaya dhidi ya Manchester City.

Beki huyo alijiunga na Napoli mwaka 2014, akitokea Saint Etienne ya nchini Ufaransa na amekwisha cheza michezo 153 katika kablu hiyo

Urusi yafungiwa kushiriki Olympiki
Makala: Saa chache za kuanika ya Kubenea, Mnyika, Sakaya ‘kutimkia CCM’