Winga wa kushoto wa Azam FC, Farid Mussa anatarajia kuelekea nchini Hispania kwa majaribio ya wiki mbili na klabu ya Slovenia, Olimpija, baada ya kupokea mwaliko wa klabu hiyo.

Nyota huyo atafanya mazoezi nchini Hispania na klabu hiyo kutoka Slovenia kwa siku kumi kabla ya kutolewa maamuzi ya kusajiliwa kwake au la.

Mabingwa hao wa Slovenia wamekita kambi ya mazoezi nchini Hispania na ombi lilitumwa juu ya nyota huyo kujiunga nao kwenye timu ya kwanza.

Afisa habari wa Azam, Jaffar Idd ameithibitisha juu ya maendeleo hayo.

“Tumemruhusu Farid kusafiri kwenda Hispania kwa majaribio na Olimpija. Kwa sasa anashughulikia viza yake na anatarajia kusafiri mapema wiki ijayo”

Farid 19, amekuwa kwenye kiwango safi kama winga wa kushoto wa Azam na Taifa Stars.

Kiwango cha kuvutia alichokionyesha katika michuano ya Kombe la Kagame mwaka huu, imefamfanya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Louis van Gaal Aendelea Kuweweseka Man Utd
Ndege yaahirisha safari Kwa Kumuogopa Panya