Saa kadhaa baada ya KMC FC kutangaza kuachana na Farouk Shikalo, Mlinda Lango huyo kutoka nchini Kenya ameibukia kwa Wakata Miwa kutoka Manungu-Tuariani Mkoani Morogoro ‘Mtibwa Sugar’.
Mtibwa Sugar wamekamilisha dili la usajili wa Shikalo katika kipindi hiki, ikiwa ni sehemu ya maboresho kikosi chao kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’.
Usajili wa Shikalo ni Dhahir unamuondoka Jeremiah Kisubi ambaye alisajiliwa kwa mkopo klabuni hapo wakati wa Dirisha Dogo la usajili msimu uliopita akitokea Simba SC.
Mbali na Shikalo, Mtibwa Sugar inaendelea kufanya usajili wa wachezaji wengine, kwa ajili ya kukiboresha kikosi chao kwa msimu mpya wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho ‘ASFC’.
Mtibwa Sugar imekua na changamoto kucheza Paly Off kwa misimu miwili iliyopita, halia mbayo imelifanya Benchi la ufundi la klabu hiyo kukisuka upya kikosi chao.
Shikalo alianza kucheza soka la Bongo akiwa na Young Africans, akisajiliwa kutoka Bandari FC ya nchini kwao Kenya, na baada ta hapo ndipo alisajiliwa KMC FC.