Watu wengi wamekuwa hawapendi kuwa na mapengo, lakini huko nchini Afrika ya Kusini hali ni tofauti, kwani mapengo ni fasheni, kama ilivyo kwa fasheni nyingine hasa kwa jamii ya Warangi, ila sio wa hapa kwetu Tanzania.

Ikiwa umewahi fika Western Cape, nchini Afrika Kusini basi utakuwa unakubaliana nami kwamba umeshawahi kuliona jambo hili dhahiri kwa macho yako watu wenye asili ya jamii ya Warangi wakiishi bila meno ya mbele.

Si kwamba walizaliwa hivyo, hapana bali waliyatoa kufanikisha mtindo ujulikanao kama ‘Passion Pengo,’ yaani wanang’oa meno ya mbele kitendo kinachochukuliwa kama ni ishara ya kudumisha mila.

Utamaduni huu, lilianza miaka 60 iliyopita, na utafiti ulionyesha kuwa asilimia 41 ya Warangi waliondolewa meno yao ya mbele, na kuingia katika dhahama ya kushindwa kula nyama kwa ustadi.

Halafu sasa cha kushangaza, Wasichana wa Kirangi huwapenda sana Wavulana wenye mapengo, yaani unaambiwa asilimia kubwa ya wakazi wana mapengo upande wa mbele, wakiamini kwamba kuondoa meno hayo ya mbele kuna thamani ya hali ya juu.

Mwenya Chipepo: Simba SC imetufunza kitu
Mikel Arteta afichua siri ya Penati