Kampuni ya ndege ya Fastjet Tanzania imewahakikishia wateja wake kuendelea kutoa huduma kwa kujiendesha yenyewe bila kutegemea msaada kutoka kwa wafadhili wao.

Mkurugenzi Mkuu Fastjet Tanzania, Derrick Luembe amesema Shirika hilo nchini linalofanya safari zake Dar es salaam, Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro, Lusaka na Zimbabwe lina vyanzo vingi vya mapato vinavyowawezesha kuendesha shirika hilo kwa kutoa huduma bora kwa wateja wake.

“Fastjet Tanzania inaweza kujiendesha. Kuna fedha nyingi kampuni itakuwa nazo kwa kujiondoa kwake Fastjet Plc. Bado tuna vyanzo vingine vya mapato kukidhi mahitaji yetu na tunaendelea kuingia mikataba mipya na wateja wetu,” alisema Luembe.

Luembe amesema hayo kufuatia taarifa iliyotolewa juzi na Fastjet Plc ya Uingereza kutaka kusitisha ufadhili wao kwa Fastjet Tanzania kutokana kukabiliwa na mapungufu makubwa ya fedha.

“Tunazungumza na wanahisa kufanya harambee kupata fedha ya ziada. Kwa hali ilivyo, Tunaweza tukasitisha huduma zetu nchini Tanzania,” ilisema menejimenti ya kampuni hiyo yenye makao yake Uingereza.

Kampuni hiyo ya usafiri nafuu wa anga imesema uamuzi wa kujitoa unatokana na changamoto za biashara zilizopo nchini hivyo majukumu yote ya uendeshaji na ugharamiaji yatabaki kwa bodi ya wakurugenzi wa Fastjet Tanzania.

Licha ya msimamo huo Fastjet Tanzania bado inaendelea kuboresha huduma za wateja wake kwani mwezi uliopita walifanya maboresha kulingana na matakwa ya wateja wao ambapo licha ya bei nafuu wanayotoza, wateja wao sasa wanapata vitafutwa na vinywaji wakiwa safarini, aliongezea Mkurugenzi wao, Derrick Luembe.

Diamond: Tunguri zimenibamba "Mobetto" - Video
Video: Major Lazer waendeleza mashavu Afrika, ni Mr Eazi na Raye ‘Tied Up’