Mahakama kuu ya Tanzania imeamua kumsimamisha wakili Fatma Karume asiendelee kuwa wakili kwa muda kufuatia kesi iliyofunguliwa na katibu Mwenezi wa ACT  Wazalendo, Ado Shaibu akipinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Fatuma Karume amesema kuwa maamuzi hayo yametolewa bila yeye kusikilizwa.

Upande wa serikali umelalamikia matamshi yaliyotolewa na wakili huyo katika kesi hiyo iliyofunguliwa dhidi ya Rais John Pombe Magufuli na mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Taarifa hiyo imetolewa na Ado Shaibu kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo amesema.

”Kesi yangu dhidi ya Rais Magufuli imeondolewa “struck out” kwa kumjumuisha Mh. “John Pombe Magufuli”. Wakili wangu Fatma Karume atafafanua.
Wakili Fatma Karume amesimamishwa (suspended) uwakili kwa maneno yake kwenye “submission” ya kutetea kesi yangu” amesema Ado Shaibu.

Uamuzi huo umetolewa leo Septemba 20, 2019 na jaji kiongozi wa Tanzania Dkt Eliezer Feleshi lakini pia ameiondoa kesi hiyo kwa sababu imemjumuisha Rais na kwa msimamo.

Fatma Karume ni mwanasheria, wakili wa kujitegemea, mwanaharakati ambaye aliwahi kuwa rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika katika kipindi cha mwaka 2018 hadi 2019.

Celine Dion ampa onyo Drake
Video: Rais Magufuli amtumbua Mkuu wa Mkoa Morogoro