Wakili wa kujitegemea, Fatma Karume ametajwa kuwa miongoni wa wagombea wa urais Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), ambapo hapo awali nafasi hiyo ilikiwa inashikiliwa na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antipas Lissu, ambaye kwa sasa yupo Ubelgiji akiendelea na matibabu baada ya kushambuliwa na risasi.
Uchaguzi huo mpya unatarajiwa kufanyika April 14, 2018 jijini Arusha, ambapo mbali na Fatma Karume wengine waliotajwa kuwania nafasi hiyo ni Makamu Rais wa TLS, Godwin Ngwilimi, Godwin Mwapongo na Godfrey Wasonga, huku Rugemeleza Nshalla akiwa amepitishwa kuwania umakamu wa urais wa chama hicho cha mawakili Tanganyika.
Taarifa hii imetolewa na Mwenyekiti wa kamati, Kibuta Ongwamuhana iliyoundwa na wajumbe watano.
-
Video: Mbowe ampa sharti Zitto, Vurugu tupu kesi ya mwanafunzi UDSM
-
Wabunge wa upinzani wafyatua gesi ya machozi bungeni
Hata hivyo Fatma ameeleza kuwa endapo atashinda na kuwa rais wa TLS, atasimamia haki, utawala bora, na atahakikishia anasimamia vyema misingi ya demokrasia inayowajibika kweli.
Aidha Machi 12, mwaka huu kamati ilikutana na kuyapitia majina yote yaliyopendekezwa na kuwateua wagombea hao kuwania kiti hiko cha urais wa Mawakili Tanganyika.